Tuesday, June 19, 2012

maisha ya wasanii bongo yanapelekwa kisanii kama kazi zao


Mwigizaji ‘five star’ kutoka tasnia ya filamu Bongo, Jacqueline Wolper Masawe, amenyang’anywa gari lake la kifahari aliokuwa akitanua nao katika mitaa mbalimbali ya jiji la Bongo.
 
Habari zenye ukweli 100% ambazo Teentz.com imezinyaka zinasomeka kuwa Wolper anayejulikana kama Amber Rose wa Bongo amenyang’anywa mkoko huo aina ya BMW X6 wenye thamani ya ‘ngawira’ za kibongo ML 170, sambamba na kupigwa ‘stop’ kukaribiana na mshefa aliyekuwa amemnunulia ndinga hiyo.

Kwa mujibu wa chanzo, hatua ya mshefa huyo kuamua kuchukua ndinga yake ni baada ya kugundua kuwa Wolper anatoka kimapenzi na ‘sharobaro’ mmoja anayemiliki duka maarufu la viwalo pande za Kinondoni.

No comments:

Post a Comment