Mwigizaji Wema Sepetu bado anaendelea kuishoot movie yake ya kwanza iitwayo
SUPER STAR ambayo inahusiana na maisha yake kwa asilimia kubwa sana, ikiwa ni
movie ambayo itaonyesha vitu vingi alivyovipitia kwenye umaarufu wake. Usiku wa
May 29 kuamkia may 30 2012 saa nane na dakika kumi ndani ya Maisha Club Dar es
salaam, Wema alivishwa pete na mwimbaji Mwinyi wa Machozi Band ambae kwenye hiyo
movie yeye atazicheza nafasi zote za Mwimbaji Diamond Platnums aliyewahi kuwa
kwenye uhusiano wa kimapenzi na Wema Sepetu, Mwinyi amecheza kama Diamond ambae
pia alimvisha Wema pete ya uchumba hapohapo Maisha Club. Akiongea Exclusive na
millardayo.com Wema amesema bajeti ya kutengeneza hiyo movie ni kuanzia milioni 29 mpaka 30 ambapo alianza
kuitengeneza march mwaka huu na ataizindua june 23 2012. Mrembo huyu ambae ni
Miss Tanzania 2006 amesema mwanzoni alikua anataka hii movie wacheze Irene Uwoya
na Jb na ilikua haikua ikihusu maisha ya Wema lakini baada ya Jb kuwa na kazi
nyingi, alifikiria kucheza movie mwenyewe na kupewa idea ya Super Star na msanii
Suma Lee. Alichofanya baada ya kupewa hiyo idea na Suma Lee ni kuipimp na
kuongeza matukio mengi aliyokutana nayo kwenye umaarufu na ni movie ambayo
mastaa wengi wa kibongo wameuza sura ndani yake
No comments:
Post a Comment